Jifunze Zaidi
Kuhusu TAMCU LTD
Chama Kikuu cha Ushirika cha Masoko ya Mazao ya Kilimo Tunduru — tangu 1994.
Historia Yetu
Historia ya TAMCU LTD
Chama Kikuu cha Ushirika cha TAMCU kilianzishwa tarehe 14.03.1994 chini ya sharia ya Vyama vya Ushirika (Sura ya 211 toleo rekebu la 2023) na marekebisho yake ya mwaka 2025 na kupewa namba ya usajili AFF-RVM-TUN-DC-2023-27.
Chama kinahusisha Vyama Vya Msingi (AMCOs) 49, ambapo Vyama Wanachama ni 44 na Vyama sio Wanachama ni 5.
1994
Mwaka wa Kuanzishwa
49
Vyama Vya Msingi (AMCOs)
44
Vyama Wanachama
5
Vyama sio Wanachama
31+
Miaka ya Huduma
Nia Yetu
Dira na Dhima
Dira
- Kuunganisha na kusajili vyama vyote vya Ushirika (AMCOS) na kuendelea kuimarisha uwezo na ufanisi wa wakulima.
- Kuakikisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo zenye tija kwa wakati.
- Kukuza na kuboresha mahusiano kati ya mkulima na mnunuzi.
- Kuendelea kuufanya ushirika wetu kuwa sauti ya wakulima na wadau wengine.
Dhima
- Dhamira yetu ni kuwa na mfumo wa ushindani na ufanisi kwenye masoko na bidhaa za kilimo.
- Kuwa nguzo ya kuboresha na kuendelea kuyapa thamini mazao ya ushirika.
- Kutoa huduma za ushauri wa masoko na bei kwa wakulima na wadau wetu.
- Kuwa chama cha Ushirika chenye ushawishi na kujenga soko la pamoja.
Eneo la Huduma
Wilaya Tunazohudumia
TAMCU LTD inahudumia vyama vya ushirika kutoka wilaya mbalimbali Tanzania.
Tunduru
35 Vyama
Wilaya ya Makazi
Namtumbo
6 Vyama
Mkoa wa Ruvuma
Songea Vijijini
1 Chama
Mkoa wa Ruvuma
Nyasa
1 Chama
Mkoa wa Ruvuma
Mbinga
1 Chama
Mkoa wa Ruvuma
Ludewa-Njombe
2 Vyama
Mkoa wa Njombe
Kyela-Mbeya
1 Chama
Mkoa wa Mbeya
Madaba
1 Chama
Halmashauri ya Mji